Diwani ya Kachenje
Mwajabu Ali Kachenje Possi (author) · T. S. Y. Sengo (introduction) · Mathieu Roy (foreword) · Jumanne Mayoka (preface) · A. Possi (illustrator)

Jahazi la ushairi la Mwajabu Ali Kachenje Possi lilianza safari yake zamani za utawala wa Waingereza katika shule ya kati ya wasichana ya Same. Likapita Korogwe na Machame, likafika Chang’ombe na Morogoro Sekondari ambako mtunzi, akiwa mwalimu wa Kiswahili, alitunga mashairi pamoja na wanafunzi wake na kushinda katika sherehe za Sabasaba. Diwani ya Kachenje ni bandari ambako jahazi hilo limetia nanga.
Mashairi yake 105, yaliyoandikwa katika kipindi cha miongo kadhaa, yanazungumzia imani na maisha ya kiroho, historia ya Taifa la Tanzania na ya Afrika, kilimo na mazingira, afya, familia, elimu, lugha na utu. Kwa mashairi ya vina na mizani na yale huru, kwa tenzi na ngonjera, mtunzi anafundisha, anaonya, anakosoa na kuhamasisha, na anahifadhi kumbukumbu za jamii na za taifa. Safari inahitimishwa na tungo tatu za Mlau alizoziandaa kwa ajili ya mahafali ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Diwani hii imetanguliwa na Zinduo la Daktari Mathieu Roy, Dibaji ya Jumanne Mayoka, na Utangulizi wa Profesa Tigiti S. Y. Sengo. Ni kitabu kwa wapenzi wa Kiswahili, kwa walimu na wanafunzi, na kwa kila msomaji anayevutiwa na uzuri wa vina na mizani.
Diwani ya KachenjeOrder the paperback, printed on demand and shipped worldwide.lulu.com